Monday, May 13, 2013

LADY JAYDEE AFIKISHWA MAHAKAMANI

 

MWANAMUZIKI Mahiri wa Bongo Fleva, Judith Wambura 'Lady Jaydee' leo alifika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam kufuatia kufunguliwa kesi ya madai katika mahakama hiyo. Katika hati ya madai hayo, mwanamuziki huyo anashitakiwa na viongozi wa Clouds Media Group ambao ni Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga. Tuhuma za kesi hiyo zinatarajiwa kusomwa mahakamani hapo na Hakimu, Athuman Nyamrani Mei 27 mwaka huu. Jaydee aliwasili mahakamani hapo akiwa na mumewe Gadner G. Habash mishale ya saa 6 mchana na kuongoza moja kwa moja chumba cha makarani wa mahakama hiyo ambao aliwakabidhi hati ya mashitaka hayo. Kwa habari zaidi na Picha za tukio hili soma http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/lady-jaydee-afikishwa-mahakamani

No comments:

Dkt. Salem Al-Junaibi na Ujumbe wake Awasili nchini kwa Ziara ya Kibiashara

Mwenyekiti wa Chama cha Biashara na Viwanda cha Oman Dkt. Salem Al-Junaibi (Mb) na ujumbe wa Wafanyabiashara wa Oman, amewasili nchini leo, ...