Monday, May 20, 2013

MRISHO NGASSA ATAMBULISHWA RASMI KUREJEA YANGA HII LEO


Katibu Mkuu wa Mabingwa wa Soka  Tanzania Bara, Yanga ya jijini Dar es Salaam, Lawrence Mwalusako amemtambulisha rasmi Mshambuliaji Mrisho Khalfan Ngassa kuwa mchezaji mpya kujiunga na timu hiyo msimu ujao wa Ligi na michuano ya kimataifa.

 
Mrisho Ngassa akiibusu jezi ya Yanga baada ya kutambulishwa rasmi kurejea katika klabu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili asubuhi ya leo, makao ya klabu hiyo makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam.

1 comment:

emuthree said...

Ndio maana nawaambia michezo sasa hivi ni biashara, nyie washabiki mnaumia wenzenu wanahesabu ....

MMUYA: WANANCHI WANUFAIKE NA UWEKEZAJI WA NHC KUPITIA NYUMBA ZA GHARAMA NAFUU

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Kaspar Mmuya, amekagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa maghala unaotekelezwa na S...