
Wabunge wa
CCM, jana walizua tafrani nje ya Ukumbi wa Bunge baada ya kukasirishwa
na kitendo cha mwenzao wa Nkasi Kaskazini, Ali Keisy kupinga Bajeti ya
Wizara ya Ujenzi wakati akichangia hotuba ya wizara hiyo.
Katika
mchango wake, Keisy alisema haungi mkono hoja kwa sababu Barabara ya
Sumbawanga hadi Kanazi-Mpanda mpaka Kibaoni haijajengwa kwa kiwango cha
lami.
Alisema
zilitengwa Sh27 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo lakini
mpaka sasa Wachina waliopewa zabuni ya ujenzi huo wamekosa fedha na
wameamua kuuza kokoto.
Mara baada
ya Bunge kuahirishwa, Keisy akiwa nje ya ukumbi huo alifuatwa na Mbunge
wa Urambo Mashariki, Profesa Juma Kapuya, Omary Nundu (Tanga Mjini),
Mendrady Kigola (Mufindi Kusini) na Rita Kabati (Viti Maalumu) na
kumzonga.Kwa habari zaidi bofya na endelea........>>>>>>>
No comments:
Post a Comment