Friday, May 31, 2013

KINANA, NAPE WAENDELEA KUMWAGA CHECHE MKOANI NJOMBE

Mkuu wa Wilaya ya Makete,Mh Josephine Matiro akimuongoza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na ujumbe wake,mapema leo mchana alipokuwa akikagua uhai wa mashina ya chama hicho katika kijiji cha Tandala,Wilaya ya Makete mkoani Njombe.Kinana na ujumbe wake wako ziarani mkoani Njombe katika kuimarisha shughuli za chama,kuangalia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi wa CCM na pia kuzungumza na Wananchi kuhusiana na matatizo yao mbalimbali yanayowakabili .
Katibu mkuu wa chama cha mapinduzi Ndugu Abdulrahman  Kinana akizungumza na Wananchi wa kata ya Iniho mapema leo jioni ndani ya wilaya ya Makete mkoani Njombe,Kinana alizungumza kwenye mkutano huo wa hadhara mambo mbalimbali ikiwemo na kuwahakikishia wananchi kuwa Serikali itaendelea kutekekeleza miradi yake yote iliyoahidi ikiwemo ya barabara,maji na umeme,aidha aliwataka wananchi kubeza baadhi ya vyama vya siasa vinanvyoeneza chuki kwa watanzania na kuindosha amani iliyopo.Kinana akiwa sambamba na ujumbe wake ameyazungumza hayo wilayani Makete katika kijiji cha Ukwama ikiwa siku ya nne ya ziara yake mkoani Njombe kutembelea mashina ya chama hicho pamoja na kufanya mikutano ya hadhara kueleza serikali ilichotekeleza.
Katibu  wa Itikadi na Uenezi Taifa  Nape Nnauye  akimtambulisha aliyekuwa mwanachama wa CHADEMA, Keffa Lupiana pichani kushoto kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo kwenye kata ya Iniho,Wilaya  ya Makete mkoani Njombe.
Mbunge wa Jimbo la Makete na Naibu Waziri wa Maji Dkt.Binilith Mahenge akieleza mambo mbalimbali ya kimaendeleo yaliyofanywa jimboni  mwake katika kutekeleza Ilani ya CCM kwenye mkutano wa .
 
 Sehemu ya Wananchi wakishangilia jambo wakati ndugu Kinana alipokuwa akizunngumza nao kwenye mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa shule ya msingi ya ukwama mapema leo jioni ndani ya wilaya ya Makete mkoani Njombe .
 
  Sehemu ya Wananchi wakiwa kwenye uwanja wa kata ya Ukwama wakimsubiri Ndugu Kinana  azungumze nao mapema leo jioni ndani ya wilaya ya Makete mkoani Njombe.
Ndugu Kinana akisalimiana akisalimiana Chifu wa kabila la Wakinga,Godfrey Mwemusi Sanga,mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara uliofanyika leo kwenye uwanja wa ukwama,wilaya ya Makete mkoani Njombe,shoto ni Katibu  wa Itikadi na Uenezi Taifa  Nape Nnauye 
 Sehemu ya hali ya hewa ya Wilaya ya Makete kama ionekavyo jioni ya leo. Picha na JIACHIE BLOG.

No comments: