Waziri Membe Amtembelea Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa Nchini Tanzania Francisco Montecillo Padilla na kumpa pole
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisalimiana na Mhe.
Francisco Montecillo Padilla, Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa
hapa nchini mara baada ya kuwasili Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam
kwa ajili ya kumsalimia na kumpa pole kufuatia shambulio la bomu
lililotokea Jijini Arusha tarehe 5 Mei, 2013 na kupelekea watu watatu
kufariki dunia na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa. Balozi Padilla alikuwa
miongoni mwa wageni waalikwa katika hafla ya ufunguzi rasmi wa Kanisa
Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, Jimbo Kuu
la Arusha wakati tukio hilo linatokea.
Mhe. Balozi Padilla akiwa katika
mazungumzo na Mhe. Membe kuhusu tukio hilo ambapo pamoja na mambo
mengine alisema kuwa anaamini suala hilo litapita na wahusika kupatikana
na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Mhe.
Membe akiagana na Mhe. Balozi Padilla mara baada ya kuzungumza
naye.Picha na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Comments