Shindano la kumsaka Malkia wa Mkoa wa Lindi ‘Miss Lindi 2013’
linataraji kufanyia Mei 31 mwaka huu katika ukumbi wa Hoteli ya Lindi Beach
Resort (Oceanic Hotel).
Akizungumza na Father Kidevu Blog mjini Lindi, Mwandaaji wa Shindano
hilo, Shaha Ramadhani kupitia kampuni ya Alliance Entertainment amesema warembo
12 wataingia Kambini Hotelini hapo chini ya Mkufunzi Zainab Mselem ambaye
alikuwa Miss Pwani 2010.
Maandalizi yote ya shindano hilo yanaendelea vyema na Milango io wazi
kwa Wadhamini kujitokeza.
Maandalizi yote ya shindano hilo yanaendelea vyema na Milango io wazi
kwa Wadhamini kujitokeza.
Irine Veda (pichani juu) ndiye anashikilia taji hilo baada ya kulitwaa mwaka 2012.
Comments