MREMBO WA REDD'S MISS TABATA 2013 KUPATIKANA LEO

Shindano la kumtafuta Miss Tabata 2013 linafanyika leo katika ukumbi wa Dar West Park Tabata. Warembo 20 watachuana kutaka kumrithi Noela Michael ambaye anashikilia taji hilo kwa sasa. Noela pia ndiye anashikiria taji la Miss Ilala.

Mbali ya kuwakilisha Miss Tabata kwenye shindano la Miss Ilala baadaye mwaka huu, mshindi huyo pia atazawadiwa Sh.600,000 pamoja na king’amuzi kutoka Multichoice ambacho kimelipiwa tayari kwa miezi mitatu kikiwa na thamani ya  Sh.400,000.

Mshindi pili atapata Sh. 300,000,  wa nne Sh.200,000 na wa tano  atazawadiwa Sh.150,000. Warembo wengine watakaofanikiwa kuingia 10 bora, watazawadiwa Sh.100,000 kila mmoja wakati waliosalia watapata kifuta jasho cha Sh.50,000 kila mmoja.

Warembo wanaoshiriki kinyang’anyiro hicho mwaka huu ni Madgalena Bhoke (21), Kabula Juma Kibogoti (20), Upendo Dickson Lema (22), Hidaya David Mwenda (22), Aneth Ndumbaro (19),  Dorice Mollel (22), Eunice Nkoha (19), Kazunde Musa Kitereja (19),  Rehema Kihinja (20),  Pasilida Mandali (21), Brath Chambia (23), Joaniter Kabunga (21), Recho Mushi (20),Caroline Sadiki (20) na  Suzan Daniel (18).

Wadhamini wa shindano hilo ni Dodoma Wine, Redd’s Original, Nipashe, Vayle Springs, Multichoice, Fredito Entertainment, Integrated Communications Limited, CXC Africa, Brake Point na Saluti5.

Miss Tabata 2013 imeandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts.

Comments