Saturday, May 25, 2013

MFUKO WA PENSHENI WA PSPF WASHIRIKI KATIKA MAONYESHO YA NANE YA VYUO VIKUU YANAYOFANYIKA DIAMOND JUBELEE DAR ES SALAAM



  
Afisa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Ndugu Ntimi Mwakajila akiwaelezea wanafunzi wa vyuo vikuu juu ya fursa mbalimbali zitolewazo na Mfuko ikiwemo mpango wa kuchangia kwa hiari.


     Mhandisi Ujenzi mwandamizi Ally Shanjirwa akielezea kuhusu nyumba zilizojengwa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF kwa ajili ya kukopesha wanachama wake.  Nyumba hizo zimekwisha jengwa katika mikoa ya Dar es Salaam, Shinyanga, Morogoro, Mtwara na Tabora.  Lakini mchakato wa ujenzi huo unaendelea katika kila mkoa Tanzania.  Nyumba hizo zinakopeshwa kwa wanachama kwa marejesho ya kila mwezi kwa muda wa miaka 25.  Mteja huyo alitembelea banda la PSPF  kwenye Mkutano wa Mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wakandalasi Mlimani City Dar es Salaam

Afisa Mwandamizi Uendeshaji Bi. Sophia Mbilikira akielezea aina mbalimbali za Mafao yatolewayo na Mfuko wa PSPF pamoja na mikopo ya nyumba.  Afisa huyo alisema sasahivi sheria inaruhusu mtu kuendeleza michango yake hata kama akiacha kazi kutoka kwa mwajiri wake alipoanzia kazi na kwenda kwa mwajiri mwengine bila kupoteza uanachama wake. Aliyasema hayo kwenye Mkutano wa Mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi Mlimani City Dar es Salaam.
 Makandarasi wa Tanzania wavutiwa na nyumba za PSPF pamoja na huduma zilizopo katika Mfuko huo.  Afisa Mwandamizi wa PSPF Bi. Sophia Mbilikira akitoa maelezo kwa wakandarasi waliokuwa wakitembelea banda la PSPF  katika Mkutano wa Mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi Mlimani City Dar es Salaam.

No comments: