Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela: “Msipokuwa makini na amani yenu, nchi hii mtaigawa vipande vipande,”


Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela
----
Kwa siku za karibuni viongozi mbalimbali wa kitaifa na wastaafu wamekuwa wakitoa matamko ya kusisitiza amani nchini.
Dodoma/Pwani.Wakati Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela ameonya Watanzania kuhusu mpasuko wa kidini akibainisha kuwa utaigawa nchi vipande vipande, Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi ametoa wito maalumu akiwataka waumini wa dini tofauti kuvumiliana.
Malecela na Mwinyi walitoa kauli hizo mjini Dodoma na Kibaha, Pwani jana kwa nyakati tofauti, wote wakiwa na nia ya kusisitiza ulinzi wa amani ya nchi inayoanza kutetereka.
Kauli ya Malecela
Malecela alisema kwa namna ilivyo sasa, Tanzania imekuwa ni tofauti na ile aliyoanza kuiona yeye katika kipindi cha uhuru kwenye miaka ya 1960 wakati huo nchi ikiwa moja na watu wake wakiwa ni wamoja.
“Msipokuwa makini na amani yenu, nchi hii mtaigawa vipande vipande na kamwe amani ya kweli haiwezi kupatikana kwa mambo ya kusingiziana, badala yake tusaidiane sisi kwa sisi, na sisi na viongozi,” alisema.Kwa Habari zaidi Bofya hapa na Endelea.......>>>>>>

Comments