Bomu Lalipuka, mmoja afa kwenye uzinduzi wa Parokia mpya ya Olasiti, Jijini Arusha leo asubuhi mpaka sasa ni majeruhi 30
Sehemu inayosadikiwa kitu kama bomu kulipuka
Baadhi ya viatu vya waumini mbalimbali waliojeruhiwa
Baadhi ya majerui wakiwa nje ya kanisa wakisubiri msaada wa kupelekwa hospitali.
Picha Juu na chini ni baadhi ya majerui wakipatiwa matibabu hospitali
Picha
juu ni baadhi ya wauminina viongozi mbalimbali wa kanisa wakiwa nje ya
kanisa muda mfupi baada ya kitu kichachosadikiwa kuwa ni bomu kulipuka
nakusababisha majeruhi zaidi ya 30 leo asubuhi.Picha Zote kwa Hisani ya
Mdau Frederick M. Katulanda
---
Na Mwandishi Wetu
MTU mmoja
ambaye hajafahamika jina lake ameuwawa, mtoto mmoja hali yake ni mbaya na
yu mahututi na wengine zaidi ya 49 wakiwa wamejeruhiwa vibaya katika
tukio la kulipuka bomu majira ya saa 5 leo asubuhi katika uzinduzi wa Parokia mpya ya
Olasiti, Jijini Arusha wakati Askofu Mkuu Josephat Louis Lebulu na Balozi wa
Baba Mtakatifu nchini, Askofu Mkuu Francisco Montecillo Padilla wakiwa wamejiandaa kuanza
maadhimisho ya misa ya kutabaruku kanisa hilo kwa kuwabariki waumini hao tayari
kwa ibada.
Taarifa za awali
zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas zinasema
kuna majeruhi zaidi ya 30, lakini wanne walikuwa na majeraha makubwa, na
amewataka wananchi kutoa ushirikiano kuweza kuwabaini waliorusha na/au kutega
bomu kwenye eneo hilo la Ibada.
Akiahirisha Ibada hiyo
Vicar General wa Jimbo Katoliki la Arusha Padre Simon Tengesi aliwataka
wakristo wote kuondoka eneo hilo na uzinduzi huo umeahirishwa hadi pale
itakapotangazwa tena, na watu wameondoka eneo hilo ili kuruhusu vyomvyo vya
ulinzi na usalama viweze kuanza uchunguzi.
Chanzo chetu cha habari
kinasema eneo lilipolipuka bomu kuna damu nyingi na watu wamejeruhiwa sehemu
mbalimbali za mwili, Tutaendelea kuwajuza zaidi.
Comments