WAZIRI wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe
----
WAZIRI wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa, Bernard
Membe ametangaza kuwa hatogomea tena ubunge katika uchaguzi mkuu ujao.
Membe ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mtama, mkoani
Lindi, alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza kwenye sherehe za Mwaka
Mpya nyumbani kwake.
“Unajua nimekuwa mbunge wenu kwa kipindi cha tatu.
Hivi leo ninawaaga rasmi kuwa sitagombea tena nafsi hii ya ubunge,”
alisema Membe.
Ambapo pia aliwataka wananchi wa mikoa ya
kusini, kuwa na subira katika kipindi hiki ambapo Serikali
inashughulikia mchakato wa kuvuna gesi asilia.Alisema kuwa ni muhimu kwa wakazi wa mikoa
iliyopatikana gesi kutambua kuwa rasilimali zilinazopatikana nchini ni
mali ya Watanzania wote na siyo ya mikoa iliyogundulika pekee.
Waziri Membe aliwataka madiwani wa Halmashauri ya
Wilaya ya Lindi, kuacha kutumia vikao vya halmashauri kujadili malumbano
yasiyokuwa na msingi akisema kwamba kufanya hivyo ni kipoteza
rasilimali za wananchi bila faida.Kwa Habari zaidi Bofya na Endelea.......
SOURCE: http://haki-hakingowi.blogspot.com
SOURCE: http://haki-hakingowi.blogspot.com
Comments