Nguzo za Zege ndani ya kituo cha Mabasi ya Ubungo Bus Terminal Jijini Dar es Salaam Zilivyoanguka Leo na Kuharibu Vibaya Magari zaidi ya 20

 Si Magari tu,hata bajaji pia zimeathiriwa vibaya kama uonavyo pichani.
Pichani juu ni baadhi ya magari mbalimbali yalioyoathiriwa vibaya kufuatia kungukiwa na ukuta.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi, KinondoniAfande Charles Kenyela akitoa maelekezo mafupi kwa baadhi ya maofisa wa Polisi waliokuwa wamefika kwenye eneo la tukio mapema leo asubuhi.Kwa picha zaidi Bofya na Endelea...........>>>>
--
Nguzo za Zege ndani ya kituo cha Mabasi ya Ubungo Bus Terminal  umeangukia magari zaidi ya 20 (baadhi kama uonavyo pichani) zikiwemo bajaji  tatu,yaliyokuwa yamepaki eneo  ambalo hutumika kupaki  wakiwa wanasindikiza abiria na ndugu zao,aidha chanzo cha ajali hiyo kimeelezaa kuwa ni Mkandarasi wa eneo hilo aliyekuwa  akibomoa ukuta huo,na pia imeripotiwa kuwa kuna baadhi ya majeruhi ambao wamekimbizwa hospitali kwa matibabu.

Comments