Wazee waasisi wa CCM kutoka mkoani Singida Wamtembelea Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula (kushoto)
akiwasikiliza Wazee waasisi wa CCM kutoka mkoani Singida, Kutoka
kushoto, Sumbu Galawa, Alhaji Mahami Rajabu Kundya na Mujengi Gwao
Makamu, walipomfikishia ujumbe wao maalum, katika Ofisi Ndogo ya Makao
Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, jana.
Mzee Sumbu Galawa akimkabidhi ujumbe maalum, Makamu Mwenyekiti wa CCM
(Bara) Pilip Mangula, wakati yeye Wazee wenzake wa CCM kutoka mkoani
Singida, Alhaji Rajabu Kundya (wapili kulia) na Mujengi Gwao (watatu
kulia) walipofika Ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM,
Lumumba, Dar es Salaam, jana, kuwasilisha ujumbe huo.
.Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Phili Mangula akimshukuru Mzee Sumbu
Galawa, baada ya kupokea ujumbe uliowasilishwa kwake na Wazee wa CCM
kutoka mkoani Singida, Ofisi jana, Ofisi Ndogo ya Makao
Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam.
Comments