Tuesday, January 22, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MAZISHI YA MAKAMU WA RAIS WA ZIMBABWE HAYATI LANDA JOHN NKOMO


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka shada la maua kwenye kaburi la Makamu wa Rais wa Zimbabwe Marehemu Dkt. Landa John Nkomo wakati wa mazishi yake yaliyofanyika jana kwenye Makaburi ya Mashujaa jijini Harare.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Mkewe Mama Asha Bilal, wakiwa katika Viwanja vya Makaburi ya Mashujaa jijini Harare, walipohudhuria maziko ya Makamu wa Rais wa Zimbabwe Marehemu Dkt. Landa John Nkomo yaliyofanyika jana jijini Harare Zimbwabwe.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akizungumza jambo na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, wakati wakiwa Ikulu ya nchi hiyo jijini Harare, jana baada ya kumaliza mazungumzo yao. Makamu wa Rais alimtembelea Rais Mugabe kwa lengo la kumfariji kutokana na kifo cha Makamu wake Marehemu Dkt. Landa John Nkomo kilichotokea mwanzoni mwa wiki iliyopita. Dkt. Nkomo alizikwa jana kwenye Makaburi ya Mashujaa jijini Harare Zimbabwe.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto) akizungumza na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe (kulia) alipomtembelea Ikulu ya Harare jana kwa lengo la kumfariji kutokana na kifo cha Makamu wa Rais wa nchi hiyo Marehemu Dkt. Landa John Nkoma, kilichotokea mwanzoni mwa wiki iliyopita na kuzikwa jana katika Makaburi ya Mashujaa jijini Harare. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Adadi Rajabu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akifurahia jambo na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, wakati akiondoka Ikulu ya nchi hiyo jijini Harare baada ya kumaliza mazungumzo yao.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
---


No comments: