Wednesday, January 16, 2013

Rais Kikwete ampokea Mwenyekiti wa AU Rais Dkt.Boni Yayi wa Benin

 
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika na Rais wa Benin, Mheshimiwa Dkt. Boni Yayi akiwasili nchini usiku wa jana, kwa ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Tanzania.

Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam, Rais Boni Yayi alipokelewa na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete mara ndege yake ilipotua kiasi cha saa tano unusu usiku.
Kesho asubuhi, viongozi hao wawili watafanya mazungumzo rasmi kabla ya Rais Boni Yayi kuondoka nchini kuendelea na ziara yake Barani Afrika.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete akimkaribisha mgeni wake Mheshimiwa Dkt.Boni Yayi wakati alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu julius Nyerere usiku wa leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Dkt.Boni Yayi wakifurahia jambo katika hoteli ya Kilimanjaro leo usiku(Picha na Freddy Maro)

No comments:

NHC YATOA ELIMU YA HATI PACHA, YASISITIZA UMOJA WA WAMILIKI SAMIA HOUSING SCHEME KAWE

 Samia Housing Scheme Kawe: nyumba 560, familia tofauti zikiunganishwa na mtindo mmoja wa maisha ya  kisasa—ushirikiano, ustaarabu na “moder...