Mtuhumiwa wa nyara za serekali Peter Laurence mwenye kofia katikati akiwa na maofisa wa jeshi la polisi chini ya ulinzi ,eneo la kisongo mtaa wa mateves nje kidogo ya jiji la Arusha baada ya kukamatwa na shehena ya nyara za serikali nyumbani kwake.
Miongoni mwa nyara za serekali zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye ghala maalumu kwenye nyumba ya mtuhumiwa Peter
Lawrence zikionekana kwenye maboksi tayari kwa kusafirishwa nje ya
nchi. (picha zote na mahmoud ahmad arusha)
********
Mahmoud Ahmad Arusha
JESHI la polisi mkoani
Arusha,limekamata shehena kubwa ya nyara mbalimbali za serikali
zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye ghala maalumu,eneo la Matevesi Kisongo
nje kidogo ya jiji la Arusha,zikiwa tayari kwa kusafirishwa nje ya nchi.
Nyara hizo ni pamoja na Ngozi za
Simba,Chui na Mamba ,meno ya Tembo,vichwa vya Nyani,Swala na Nyati,Pembe
za kifaru,na zingine nyingi ambazo jeshi la polisi linaendelea
kuzitambua.
Sambamba na hilo jeshi hilo
limemtia mbaroni mtuhumiwa wa nyara hizo aliyetambulika kwa jina la
Peter Leurence (55)mkazi Ngaramtoni ya chini,ambaye alikuwa akiwa
amezihifadhi kwenye maboksi zaidi ya 20,kwenye nyumba yake iliyopo eneo
hilo.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi
mkoni Arusha,Liberatus Sabas tukio la kukamatwa kwa nyara hizo limetokea
jana majira ya saa 6.30 usiku wa kuamkia leo eneo la kisongo mtaa wa
mateves baada yak upata taarifa kutoka kwa raia wema.
Kamanda Sabas alisema kuwa baada
ya jeshi hilo kupata taarifa za siri majira ya saa 5 asubuhi walifika
eneo la tukio majira ya saa 7 mchana na kupata upinzani mkubwa kutoka
kwa walinzi wa wanaolinda eneo hilo kwani waliwanyima kuwapa maelekezo
ya kumpata mmiliki wa nyumba hiyo.
Hata hivyo alisema kwamba askari
hao waliamua kumueka chini ya ulinzi kwa kumshurutisha mlinzi mmoja
iliaweze kuwapa ushirikiano ambapo aliwapaita namba za simu na mtuhumiwa
aliwaambia kuwa yupo magugu mkoani Manyara na angefika saa 12 majira ya
jioni.
Taarifa zinadai kuwa baada ya
mtuhumiwa kufika jitihada za kufanya upekuzi zilifanyika chini ya polisi
wenye silaha za moto na walikuta shehena kubwa ya nyara za serekali
zilizokuwa zimahifadhiwa kwenye ghala maalum na kufungwa kwenye mabox
teyari kusafirishwa kwenda kusikojulikana.
Alisema kuwa polisi waliamua
kuweka ulinzi hadi kulipokucha na huku wakiendelea kumshikilia mtuhumiwa
huyo na jeshi hilo linaendelea kumshikilia mtuhumiwa huyo pamoja na
watoto wake wawili waliokutwa wakiishi kwenye nyumba hiyo.
Aidha kamanda Sabas alisema kuwa
kesho yake polisi waliendelea kufanya upekuzi na kubaini mabox zaidi ya
20 yenye nyara mbali mbali miongoni mwa nyara hizo alizitaja kuwa ni
Ngozi za Chui.Simba,Tembo na Mamba pia kulikuwemo vichwa vya
nyani,chui,swala nyati,pembe za faru ,meno ya tembo na nyingine nyingi
ikiwemo mfuko wa silaha inayosadikiwa kuhifadhia silaha.
Kwa mujibu wa kamanda wa jeshi la
polisi mkoani hapa alisema kuwa Watuhumiwa bado wanashikiliwa na jeshi
hilo kwa mahojiano na watafikishwa kwenye mahakama pindi upelelezi wa
tukio hilo utakapo kamilika.
Comments