Thursday, January 24, 2013

Video ya Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Chadema, Benson Kigaila Akimjibu Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi-CCM, Nape Nauye


--
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimejibu CCM kuhusu kauli zake za hivi karibuni kuwa Chadema itakufa.Akihutubia Mwanza hivi karibuni, Nape Nnauye alikaririwa akisema Chadema itakufa kutokana na laana ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na kwamba ni chama kilichojaa ubaguzi.

Akijibu kauli hiyo jana, Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Chadema, Benson Kigaila alisema chama hicho hakiwezi kulumbana na Nape.

Kigaila alisema Chadema haina makundi na haitakufa kwa laana ya Mwalimu Nyerere.
“Tunataka kuwaambia kuwa Chadema haina ubaguzi hivyo haiwezi kufa leo wala kesho mpaka iwe imetimiza kazi yake ya kuwakomboa Watanzania. Kama ni suala la Mwalimu Nyerere, laana hiyo iko ndani ya CCM yenyewe,” alisema.

Akitaja sababu za kudai kuwa laana imo ndani ya CCM, Kigaila alisema chama hicho kimevunja umoja wa kitaifa uliojengwa na Mwalimu Nyerere na kwamba, alitunga kitabu kuwa CCM imeoza na kinanuka rushwa.
Aliongeza kuwa CCM ina laana ya Mwalimu kwa sababu imerasimisha ubaguzi kwa viongozi wanachama wao.

“Ni haohao CCM wanaosema Chadema kina ukabila waliomzushia Dk Salim Ahmed Salim uongo kuwa ni Mwarabu na alihusika na kifo cha aliyekuwa mmoja wa waasisi wa taifa hili, Abeid Karume. Uchafu uliofanywa na wanamtandao,” alisema Kigaila.


Aliendelea kuituhumu CCM kwa kukandamiza haki za wafanyakazi, huku akitoa mfano wa tukio la kutekwa na kuteswa kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania (Mat), Dk Steven Ulimboka.Kwa Habari Zaidi Bofya na Endelea.....>>>>

No comments: