Tuesday, January 29, 2013

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana na Sekretarieti Nzima ya CCM Watembelea ujenzi wa daraja la Malagarasi

Katibu Mkuu wa CCM Abdurahaman Kinana akihutubia ngaruka
 Dk Asha-Rose akihutubia Nguruka
Nape Nnauye akihutubia Ngaruka
Kinamama katika mji mdogo wa Nguruka wilayani Uvinza mkoani Kigoma, wakipokea kwa shangwe msafara wa Kinana na ujumbe wake ulipowasili kwa ajili ya mkutano wa hadhara.
 Juma Kilabuka na Hasani Kankwi wa mjini mdogo wa Nguruka wakifurahia msafara wa Kinana ulipofika katika mji huo
Kinana akisalimia wananchi katika mji mdogo wa Nguruka , Uvinza mkoani Kigoma baada ya msafara wake kuwasili  katika mji huo kwa ajili ya mkutano wa hadhara.
Dk. Asha Rose Migiro akishangiliwa na mkazi wa Nguruka,  Asha Kipenda wakati wa mapokezi ya msafara wa Kinana na ujumbe wake ulipowasili Nguruka mkoani Kigoma, Januari 28, 2013.
Kinana akiaga wananchi baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Nguruka, wilayni Uvinza mkoani Kigoma. Kushoto kwake ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro
Dk. Asha Migiro akiwa katika matembezi kuingia mjini mdogo wa Nguruka wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma,kwenda kwenye mkutano wa hadhara wa CCM. Kushoto ni Asha Baraka.
Nape akishiriki kupiga ngoma ya kuongoza matembezi kuingia mji mdogo wa Nguruka, wilayani Uvinza mkoani Kigoma, kwenda kwenye mkuytano wa hadhara wa CCM, Nguruka, Januari 28, 2013. Pembeni yake ni Asha Baraka
Meneja mradi wa ujenzi daraja la Malagarasi wa Kampuni ya Korea ya Hanil, Jung Sik You, (wapili kushoto) akimtembeza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (watatu kushoto) na ujumbe wake kushuhudia hali ya ujenzi wa daraja hilo ilivyo, Januari 28, 2013, wilayani Uvinza mkoani Kigoma. Kwa mujibu wa You mradi huo umekamilika kwa asilimia 85 na unatarajiwa kukamilika  Aprili mwaka huu. Wengine ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (wanne) na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (wapili kushoto) . Kinana na ujumbe wake wapo mkoani Kigoma kwa ajili ya kushiriki kwenye kilele cha sherehe za miaka 36 ya CCM zitakazofanyika Januari 3, 2013.
Kinana akizungumza na mwananchi wa Kigoma Amani Khalidi wakati akikagua ujenzi wa daraja la Malagarasi. kushoto ni  Meneja mradi wa ujenzi daraja la Malagarasi wa Kampuni ya Korea ya Hanil, Jung Yong.Picha Zote na Bashir Nkromo-Idara ya itikadi na Uenezi-CCM
----
CHAMA Cha Mapinduzi(CCM), kimesema kuwa wananchi wa Mtwara wanayo hoja hivyo Serikali inatakiwa kuwasikiliza na kutoa majibu sahihi.

Pamoja na hayo chama hicho kimesema kuwa kinachoonekana hivi sasa nyuma ya sakata hilo kuna watu wanafanya uhaini, uhalifu na kila aina ya hujumu jambo ambalo wanaitaka Serikali kuchukua hatua kali za kuhakikisha wote wanojihusisha na uhalifu huo wanachukuliwa hatua.

Kauli hiyo ilitolewa jana mjini hapa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana ikiwa ni msimamo wa chama chao katika sakata hilo.

Mjadala wa gesi ya Mtwara kutoka mkoani humo kwenda Dar es Salaam umekuwa gumzo kubwa huku wananchi wakiitaka Serikali kuwaeleza watanufaika vipi na gesi hiyo kabla ya kunufaisha maeneo mengine.

Kinana alisema kuwa kuna haja kwa Serikali kuhakikisha inatumia nafasi yake kuzungumza na wananchi wa Mtwara katika kupata suluhu ya suala hilo kwani wana hoja za msingi ambazo zinataka majibu.

“Msimamo wetu kama chama, tunataka Serikali kukaa na wananchi hao na kuwasikiliza.Tunahitaji kuona Serikali inatoa majibu ambayo yatakuwa sahihi na kumaliza tofauti iliyopo sasa,”alisema Kinana.

Pamoja na hayo alisema kuwa kinachoshangaza ni kuona hali ya uvunjifu wa amani inayofanywa na baadhi ya watu ambao wameamua kuingia mtaani na kuiba, kupora mali na kuharibu nyumba za watu kwa kuzichoma moto.

Alisema kuwa CCM inaona ni wakati mzuri kwa Serikali kuwadhibiti wote ambao wanatumia mwanya huo kufanya uhalifu huo ambao haukubaliki huku akisisitiza umuhimu wa wananchi kusikilizwa.

Alisema mtazamo wa chama chao ni kwamba kuna jambo ndani ya suala hilo maana gesi inatakiwa kujadiliwa kwa njia ya amani kupata suluhu kuliko mali za watu kuharibiwa na kufanywa kwa uhalifu ambao hauvumiliki.

No comments: