Maendeleo ya msiba wa Sajuki nyumbani kwao Tabata Bima

Baadhi ya Wasanii wa Filamu nchini wakiwa kwenye msiba wa Msanii mwenzano,Marehemu Sadick Juma Kilowoko ama Sajuki aliefariki Dunia mapema leo asubuhi,kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu.taratibu za Mazishi ya Sajuki zinakwenda vizuri na Mwenyezi Mungu akijaalia Siku ya Ijumaa,Marehemu Sajuki  atasikwa kwenye Makaburi ya Kisutu jijini Dar,Majira ya Saa tano asubuhi kwa mujibu wa mtoa taarifa.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi an Teknolojia Mh. January Makamba (mwenye fulana ya njano) akisikiliza maelezo ya juu ya maendelea ya Msiba wa Msanii Sadick Juma Kilowoko a.k.a Sajuki aliefariki dunia leo kwenye Hospital ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa.Taarifa hiyo ilikuwa ikitolewa na Rais wa Shirikisho la Wasanii wa Filamu Tanzania (TAFF),Saimon Mwakifwamba
Wasanii wa kila wa tasnia mbali mbali hapa nchini wakiwa msibani hapo.
Waombolezaji wenginwa wakiwa wamekaa kwenye mtaro
Mazungumzo ya hapa na pale.
Rais wa Shirikisho la Wasanii Tanzania (TAFF),Saimon Mwakifwamba (kushoto) akizungumza na baadhi ya waombolezaji wengine msibani hapo.
Waombolezaji wa msiba wa Sajuki wakiwa Nyumbani kwa Marehemu.
Kisomo kikiendelea.

Comments