Sunday, January 27, 2013

RAIS KIKWETE AHUDHURIA MKUTANO WA AU


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa ufafanuzi kuhusu hoja mbalimbali zilizoibuliwa na jopo la APRM kuhusu Demokrasia na Utawala Bora nchini Tanzania. Mhe. Rais alitoa ufafanuzi huo mbele ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Mhe. Rais Kikwete (kushoto) akibadilishana mawazo na Mhe. Salum Barwany, Mbunge wa Jimbo la Lindi Mjini nje ya ukumbi wa mkutano nchini Ethiopia.
Mhe. Jacob Zuma, Rais wa Afrika Kusini na Mhe. Paul Kagame, Rais wa Rwanda nao walihudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa AU ambapo Tanzania iliwasilisha ripoti yake kuhusu Demokrasia na Utawala Bora. Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiendelea kutoa ufafanuzi kuhusu masuala ya Demokrasia na Utawala Bora nchini Tanzania. Wengine katika picha ni Waziri Bernard K. Membe (Mb) (wa pili kulia), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, wakiwemo pia wajumbe na Wabunge waliofuatana na Mhe. Rais Kikwete kuhudhuria Mkutano huo.

No comments:

DKT. ABBASI AKAGUA MIRADI YA UTALII PORI LA AKIBA LA PANDE, ATOA MAAGIZO YA KUKAMILIKA KABLA YA AFCON 2027

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, leo Julai 23, 2026, ametembelea Pori la Akiba la Pande jijini Dar es Salaa...