Wednesday, January 16, 2013

MANJI ACHUKUA FOMU TFF, KUMEKUCHA



Manji anazungumza na Waandishi wa Habari baada ya kuchukua fomu
Mmiliki wa klabu ya African Lyon, Rahim Kangenzi ‘Zamunda’ akimchukulia fomu ya kugombea Uenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu kwa niaba ya klabu za Ligi Kuu zilizompendekeza, Mwenyekiti wa Yanga SC, Yusuf Mehbub Manji (kulia) ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ilala, Dar es Salaam mida hii, kuelekea uchaguzi utakaofanyika Februari 24, mwaka huu mjini Dar es Salaam. Anayetoa fomu hiyo kushoto ni Ofisa wa TFF, Jonathan Aloyce Kakwaya.   
Zamunda anamkabidhi fomu yake Manji
Mhasibu wa TFF anamuandikia Manji risiti

MALINZI AREJESHA FOMU YA KUOMBA URAIS TFF, ALICHUKUA KWENYE MTANDAO

Mwenyekiti wa Chama cha Soka Kagera (KRFA), Jamal Emil Malinzi akirejesha fomu ya kugombea urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ofisi za shirikisho hilo, Ilala, Dar es Salaam mida hii, kuelekea uchaguzi utakaofanyika Februari 24, mwaka huu mjini Dar es Salaam. Anayepokea fomu hiyo ambayo Malinzi alichukua kwenye tovuti ya TFF na kujaza kisha kuilipia katika benki ya CRDB kushoto ni Ofisa wa TFF, Jonathan Aloyce Kakwaya.   
Anashuka kwenye gari

Anaanza kuekelea ofisi za TFF
Anajiorodhesha
Risiti yake ya benki

Anazungumza na Waandishi wa Habari. Picha na habari zote za  http://bongostaz.blogspot.com/2013/01/manji-naye-achukua-fomu-tff-kumekucha.html

No comments: