Monday, January 14, 2013

Sakata la gesi Mtwara: James Mbatia na Wabunge Wake Wakatisha Hotuba Zao Baada ya Kuanza Kurushiwa Chupa tupu za Maji baada ya Kuanza Kusema Kwenye Mkutano wa Hadhara Mtwara..


MWENYEKITI wa NCCR Mageuzi, James Mbatia
---
MWENYEKITI wa NCCR Mageuzi, James Mbatia jana alijikuta katika wakati mgumu baada ya kulazimika kufungiwa katika ofisi ya NCCR-Mageuzi wilaya ya Mtwara Mjini kutokana na baadhi wa wananchi walioudhuria mkutano wake wa hadhara uliofanyika uwanja wa Mashujaa, kutaka kumdhuru kwa madai kwamba hawakuridhishwa na hotuba yake.

Mbatia alianza kurushiwa chupa tupu za maji alipokuwa akitoka uwanjani hapo baada ya kukatisha hotuba yake kutokana na baadhi ya wananchi kupinga kauli zake kwa madai hawamuelewi.

 Kauli inayodaiwa kumgharimu Mbatia ni ile ya ‘Iwapo gesi itatoka Mtwara’ ndipo wananchi hao walipoanza kupaza sauti wakisema “Hatukuelewi…hatukuelewi” hata hivyo Mbatia aliendelea kuhutubia hali iliyosababisha wananchi hao wapaze sauti zao kwa kuimba nyimbo.

“Haitoki… Hatoki…Haitoki…” sauti za wananchi zilisikika na hata Mbatia alipojaribu kuwatuliza wananchi hao kwa kusema ‘gesi kwanza…. Gesi kwanza” baadhi waliitikia na wengine waliendelea kusema hawamuelewi.
Hali hiyo ilimlazimisha Mbatia kukatisha hotuba yake saa 11.25 jioni na aliondoka uwanjani hapo kwa kutembea kwa miguu hali iliyotoa mwanya kwa wananchi kumrushia chupa tupu za maji. Mwenyekiti huyo akiwa ameambatana na wabunge wa chama hicho, Moses Machali (Kasulu Mjini) na Agripina Buyogela (Kasulu Vijijini) mkoani Kigoma, walielekea kituo cha polisi kilichopi karibu na uwanja huo na baadaye alielekea ofisi za NCCR Mageuzi wilaya.Kwa habari zaidi Bofya na Endelea......>>>>

1 comment:

Anonymous said...

Msikaji ni kibaraka wa CCM lazima wana wammaindi Sana tu