Sunday, January 27, 2013

SEKRETARIETI YA CCM YAWASILI KWA TRENI MKOANI KIGOMA

Katibu Mkuu akizungumza na wananchi wa Kigoma
Sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imewasili salama mkoani Kigoma ikitokea jijini Dar es Salaam kwa njia ya Reli.
Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM, wakiongozwa na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana (wapili kulia) akimpongeza Dereva wa Treni aliyewafikisha Mjini Kigoma salama. Wengine pichani kutoka kushoto ni Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye , Katibu wa Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Hajati Dk. Asha-Rose Migiro na Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela
Wananchi wakisogea kuwapokea viongozi *********************************** Sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imewasili mkoani Kigoma ikitokea jijini Dar es Salaam kwa njia ya Reli. Wakipokelewa kwa Shangwe, takribani kila kituo njiani, Sekretarieti hiyo iliyoongozwa na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana pamoja na wajumbe wengine ambao ni Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, Katibu wa Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Hajati Dk. Asha-Rose Migiro na Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela uliwasili Mjini Kigoma majira ya saa nne asubuhi na kupokelewa na Wakazi wa mji wa kigoma. Akizungumza baada ya kuwasili Kigoma, Katibu Mkuu wa CCM, Kinana alisema yakuwa leongo la safari yao hiyo ya Treni ni kuwadhihirishia wakazi wa Kigoma na taifa kwa Ujumla kuwa Usafiri wa Treni ni wa uhakika na Serikali ya Chama cha Mapinduzi kupitia Wizara ya Uchukuzi kuanzia sasa itasimamia kikamilifu usafiri huo na kuboresha huduma maradufu na kuhakikisha safari zinaongezeka. Nao baadhi ya wakzi wa Mkoa wa Kigoma wameipongeza sana Sekretarieti hiyo kwa uamuzi wa kusafiri kutoka jijini Dar es Salaam hadi Kigoma kuhudhuria maadhimisho ya miaka 36 ya CCM kwa treni na kudai kuwa kufanya hivyo ni uzalendo tosha na kuonesha haki kwa wananchi wote.SOURCE: MROCKY MROCKY

No comments: