Monday, January 14, 2013

Wanafunzi wa Chuo cha IFM waandamana katika Ofisi Wizara ya Ndani! Kamanda Kova awasili kutuliza Vurugu



Wanafunzi wa Chuop Cha Uongozi wa Fedha cha jijini Dar es Salaam (IFM) wakiwa mbele ya geti la Wizara ya Mambo ya ndani walipovamia leo majira ya saa nne na nusu asubuhi wakiwa na madai ya kutopewa ulinzi na jeshi la polisi kwenye makazi yao ya Hosteli za Kigamboni kutokana na kuvamiwa na majambazi mara kwa mara. Wanafunzi hao walidai siku ya Ijumaa walifanya kikao na jeshi hilo ili wawape ulinzi lakini suala la ajabu siku waliyofanya kikao na Jeshi hilo ndio siku waliovamiwa wenzao wawili wakiume na kubakwa  hali iliyosababishwa wanafunzi hao kubakwa. Majambazi hao wamekua wakidai kupewa Laptop simu na fedha kama mwanafunzi akikataa humfanyia vitendo vya kulawiti.
Ulinzi uliimarishwa nje ya jengo la Wizara ya Mambo ya ndani kufuatia kadhia hiyo ya wanafunzi.

Kamanda wa Polisi wa Kanda maalum ya Kipolisi ya jiji la Dar es Salaam Suleiman Kova akimsikiliza Rais wa Serikali ya wanafunzi ya Chuo cha IFM mara baada ya kuwasili eneo la ofisi za Wizara ya Mambo ya ndani ambapo aliwaamuru wanafunzi hao wafuatane waende hadi Kigamboni kwenye Kituo walichoripoti taarifa zao pamoja na kwenda kwenye Hosteli zao. Kova aliahidi kushughulikia jambo hilo kwa haraka bila kusita.
"Wanafunzi wenzetu wa kiume wamelawitiwa nyinyi tumewapa taarifa siku ya ijumaa kuwa hatuna ulinzi tunaibiwa hovyo vitu vyetu halafu siku hiyo hiyo unafanyika ubakaji huo"

Baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye mitaa ya Posta jijini humo wakielekea kwenye kivuko cha Kigamboni ili kwenda kumuonyesha Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Kipolisi ya jiji la Dar es Salaam Suleiman Kova.
Wakianza maandamano kuelekea Feli kwaajili ya kuvuka kwenda Kigamboni.
Kova akitoa maelezo kwa waandishi wa habari juu ya hatua zitakazochukuuliwa baada ya kupata taarifa hizo ambapo aliwaamuru wanafunzi hao wote kwapamoja kwenda Kigamboni kufuatilia tukio hilo kwa pamoja.
Mitaani Posta.
Hadi kieleweke!
Tunaimba! Tunavuka bure Tunavuka bure kwenye Pantoni.
Kova akishangiliwa wakati wa safari kuelekea Feli.
Kwenye Kona ya feli kuwania geti ili waingie bure!
Wakajazana kupita kiasdi Kova akazuia kivuko kisiondoke hadi wapungue!
Hapa wakigoma kupungua kazi iliyochukua zaidi ya Saa moja hadi kivuko kuendelea na kazi ya kuvusha abiria
Pamoja na kutakiwa kupungua hapa wengine walizidi kuendelea kuingia na kukijaza kivuko hicho. Picha zote na Raha za Pwani, hii ni sehemu ya kwanza tutawaletea sehemu ya pili ya tukio hili ambalo hadi hivi sasa filamu inaendelea hapa feli na ikielekea Kigamboni. Picha zote Kwa Hisani Ya Mtaa Kwa Mtaa Blog


Wanafunzi wa Chuo cha IFM wakiwa nje ya Ofisi ya Wizara ya mambo ya nje ambapo ndipo wamefikia kwa Maandamano yao
kwa picha zaidi

No comments: