Thursday, January 31, 2013

DR. ASHA ROSE MIGIRO ATEULIWA KUWA MKUU WA CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dkt. Asha Rose Migiro kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Taarifa iliyotolewa Dare Es Salaam na kutiwa saini , Jumatano, Januari 30, 2013 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza Alhamisi ya Januari 17, mwaka huu wa 2013.


Mheshimiwa Asha Rose Migiro ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Katibu wa NEC wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.


Aidha, Dkt. Migiro amepata kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania. 


Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
DAR ES SALAAM
30 Januari, 2013

No comments:

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AMTEMBELEA MHE. FARIDA AMOUR MOH'D HOSPITALINI, AMTAKIA AFYA NJEMA

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla , leo tarehe 21 Mei 2026 amemtembelea na kumjulia hali Mwakilishi wa Viti M...