Waziri
 wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka 
akiwasalimia wakazi wa kata ya Bunju na Wazo mara baada ya kuwasili 
katika eneo  hilo  kwa lengo la kuzungumza nao ili kutafuta suluhisho la
 kudumu la  mgogoro wa ardhi kati yao na  kiwanda cha Saruji cha Twiga 
jana jioni.
(PICHA NA ARON MSIGWA WA MAELEZO)
Waziri
 wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka akiongea 
katika mkutano wa hadhara na maelfu ya wakazi wa kata ya Wazo na Bunju 
waliojitokeza kufuatilia maendeleo ya mgogoro wa ardhi kati yao na 
Kiwanda cha Twiga Cement ambapo pamoja na mambo mengine amewahakikishia 
wakazi hao kuwa mgogoro huo utapatiwa ufumbuzi wa kudumu na kuwaomba 
kutoa ushirikiano kwake.
Diwani
 wa eneo la Bunju na Wazo Sharif Exavery Majisafi akiongea na wananchi 
kabla ya kumkaribisha Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi 
Prof. Anna Tibaijuka kuzungumza nao.
Sehemu
 ya umati mkubwa wa wakazi wa kata za Bunju na Wazo wakimsikiliza kwa 
makini Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna 
Tibaijuka.
Waziri
 wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka akipitia 
baadhi ya nakala za ramani zinazoonyesha eneo la Kata ya Bunju na Wazo 
pamoja na Kiwanda cha Saruji cha Twiga ambazo ziligawiwa kwa wananchi. 
Kushoto ni Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na
 Maendeleo ya Makazi Dkt. Silasi Mayunga
Waziri
 wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka (kulia) 
akiongea na Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha Saruji cha Twiga (Twiga 
Cement) Bw.Pascal Lessoinne (kushoto) mara baada ya mkurugenzi huyo 
kutoa taarifa fupi ya maendeleo ya kiwanda hicho na hali ya mvutano wa 
muda mrefu wa umiliki wa maeneo baina ya wakazi wa kata za Bunju na Wazo
 jijini Dar es salaam.
Katika
 hali isiyokuwa ya kawaida kijana mmoja ambaye jina lake halikuweza 
kupatikana mara moja  katikati ya wananchi wenzake akiwa amevaa kofia 
ngumu ya waendesha pikipiki wakati wa mkutano wa hadhara wa wakazi wa 
kata ya Bunju na Wazo na Waziri wa Ardhi Prof. Anna Tibaijuka kujadili 
mgogoro wa ardhi kati yao na Kiwanda cha Twiga Cement. Haikujulikana 
mara moja lengo la kuvaa kofia hiyo licha ya mkutano huo kutawaliwa na 
amani na maelewano makubwa.







 
 
No comments:
Post a Comment