Posted by
Vempin Media Tanzania
on
- Get link
- X
- Other Apps
Louise Kamin Meneja Mradi wa
Media For Development International Tanzania akizungmza kuelezea filamu
ya Siri ya Mtungi ilyotengenezwa na taasisi hiyo itakayokuwa ilirushwa
na vituo vya televisheni vya ITV na EATV ikiwa na maudhui ya maisa
katika familia ya jamii inayohamasishwa na penzi,
lililoletwa na woga, ushirikina na usaliti, ikinyanyuliwa na
ucheshi na furaha, na kupewa nguvu ya mshikamano wa ndani wa
familia na urafiki. Uzinduzi wa filamu hiyo ulifanyika jana kwenye
ofisi za shirika hilo Msasani jijini Dar es salaam
Baadhi ya waandishi wa habari na
wageni walioalikwa katika uzinduzi huo uliofanyika katika ofisi za
shirika hilo Msasani jijini Dar es salaam.
Baadhi ya washiriki waliocheza katika filamu hiyo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi huo jana.
………………………………
Tamthilia mpya kabisa ya Televisheni kutoka kwa Watu wa Marekani! Onyesho la Kwanza la SIRI YA MTUNGI litakuwa
ITV saa 3.30 usiku tarehe 9 Desemba. Na EATV saa 3.30 usiku tarehe 12 Desemba.
Mchanganyiko mzuri wa wahusika wa Siri ya Mtungi, waliohusiana kwa damu au ndoa, au kwa mapenzi tu, unaunda
jamii inayohamasishwa na
penzi, lililoletwa na woga, ushirikina na usaliti, ikinyanyuliwa
na ucheshi na furaha, na
kupewa nguvu ya mshikamano wa ndani wa familia na urafiki.
Tamthilia hii ya Televisheni
ni Programu ya awali ya TCCP (Tanzania Communications
Capacity Project) iliyotekelezwa
na JHU-‐CCP (Johns Hopkins Bloomberg School of Public Health Center for Communications Programs) kwa msaada
wa USAID (United States Agency for International Development) na kama sehemu ya PEPFAR (US President’s
Emergency Fund for AIDS Relief).
Ikiwa imetayarishwa na MFDI (Media For Development International), Siri ya Mtungi inawaleta pamoja Wasanii bora
wa Tanzania, waandishi, wana mitindo ya nguo, wakurugenzi wa sanaa, waigizaji na watendaji wa filamu kwenye
mafanikio makubwa ya ukuaji wa tasnia ya filamu na televisheni Tanzania.
Kati ya mitaa yenye harakati
nyingi ya Dar es Salaam na ile iliyo kimya ya Bagamoyo,
tunapenya nyuma ya milango
iliyofungwa mpaka kwenye maisha ya Cheche na mkewe Cheusi, binti wa kiongozi maarufu katika jamii, mwenye
wake wengi, Mzee Kizito,
pamoja na wahusika wengine kama Duma, mwana DJ; Lulu-‐
shangingi lililokubuhu; Farida-‐
roho ya nyoka; Masharubu-‐ mzee kikwekwe na wengine wengi.
RATIBA YA ITV: Jumapili 3.30 usiku -‐ Jumatano 3.30 usiku
RATIBA YA EATV: Jumatano 10.30 Alasiri -‐ Alhamisi 7.00 Mchana -‐ Jumamosi 10.30 Alasiri
Comments