GAZETI JIPYA LA MATANGAZO LINALOITWA DAR METRO LAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM

 
Bw. Juma Pinto Mtendaji Mkuu  wa Kampuni ya Jambo Concept (T) Limited kushoto akiwa pamoja na Lightness Sirikwa Meneja Matangazo na na Mhariri Mkuu Yakobe Chiwambo wakionyesha gazeti jipya la matangazo la Dar Metro lililozinduliwa jana katika mgahawa wa City Sports Lounge Posta jijini Dar es salaam jioni ya jana, ambapo wadau kutoka makampuni mbalimbali yanayojihuzisha na biashara ya matangazo wamehudhuria katika hafla hiyo, gazeti hilo litagawiwa bure katika maeneo mbalimbali ya kibiashara jijini Dar es salaam  na mikoani hapa nchini
 
Bw. Juma Pinto Mtendaji Mkuu  wa Kampuni ya Jambo Concept (T) Limited akizungumza na wageni waalikwa wakati alipozindua rasmi gazeti la matangazo linaloitwa Dar Metro kwenye mgahawa wa City Sports Posta jijini Dar es salaam, katikati ni Peter Ambilikile Mwandishi mwandamizi wa gazeti la Dar  Metro na kulia ni Lightness Sirikwa Meneja Matangazo wa gazeti la Dar metro
 
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts (T) Limited Mzee Ramadhan Kibanike akizungumza katika uzinduzi huo
 
Wafanyakazi wa Kampuni ya Jambo Concepts na wadau mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye mgahawa wa City Sports Lounge jijini Dar es salaam.

Comments