Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama, Rais Jakaya Kikwete 
akizungumza na wananchi wakati wa maadhimisho ya sherehe  za miaka 51 ya
 Uhuru wa Tanganyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. 
Rais
 wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dk.Jakaya 
Kikwete akiwasili katika gari maalum la Kijeshi na Mkuu wa majeshi 
Jenerali Davis Mwamunyange kwenye uwanja wa uhuru kwa ajili ya  
maadhimisho ya miaka 51 Uhuru wa Tanzania Bara 2012 yanayofanyika kila 
mwaka Desemba 9, Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Mwaka huu ni “Uwajibikaji,
 Uadilifu na Uzalendo ni nguzo ya Maendeleo ya Taifa letu”
(PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWEBLOG.COM)
Amiri
 Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania Dk. Jakaya 
Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya Ulinzi na usalaama katika 
maadhimisho hayo.
Amiri
 Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania Dk. Jakaya 
Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya Ulinzi na usalaama katika 
maadhimisho hayo
Kikosi cha Brass Band cha majeshi ya Ulinzi na usalama  kikitumbuiza katika maadhimisho hayo

Viongozi mbalimbali wakiwa katika 
maadhimisha hayo kutoka kulia ni Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya 
Kidemokrasia ya Congo, Mama Maria Nyerere, Rais wa Msumbiji Mh. Armando 
Guebuza,Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Gharib 
Bilal na Mzee Ali Hassan Mwinyi rais Mstaafu wa awamu ya pili
Rais
 wa Msumbiji Mh. Armando Guebuza akipokewa  na Mkuu wa mkoa wa Dar es 
salaam Mh Said Meck Sadik mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Taifa.
Rais
 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mh. Joseph Kabila akipokewa  na 
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Said Meck Sadik mara baada ya kuwasili 
kwenye uwanja wa Uhuru asubuhi hii.
Mama Maria Nyerere akiwasili kwenye uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kuhudhuria maadhimisho ya miaka 51 ya uhuru wa Tanzania.
Waziri
 Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Mizengo Pinda akiwasili 
kwenye uwanja wa Uhuru kuhudhuria maadhimisho hayo huku akisindikizwa na
 Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Said Meck Sadik.
Mzee Ali Hassan Mwinyi akiwasili kwenye uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kuhudhuria maadhimisho hayo.
Vikosi
 vya Ulinzi na Usalama vikiwa vimejipanga tayari kwa gwaride  la utii na
 heshima mbele ya Amiri jeshi Mkuu na Rais Jamhuri ya muungano ya 
Tanzania Dk. Jakaya Kikwete.
Makamu
 wa Rais Dk. Gharib Bilal akisalimiana na Mama Fatma Karume mara baada 
ya kuwasili uwanjani hapo, katikati ni Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda.
Rais
 Jakaya Kikwete akipokea gwaride la heshima wakati wa maadhimisho ya 
miaka 51 ya uhuru wa Tanzania Bara yanayofanyika kwenye uwanja wa Uhuru 
jijini Dar es salaam akiwa pamoja na viongozi mbalimbali kutoka nje na 
ndani ya nchi
Rais
 Dk. Jakaya Kikwete kulia akipokea Gwaride la Heshima lililpokuwa 
likipita mbele yake wanaofuatia katika picha ni Rais wa Zanzibar Dk. 
Mohamed Shein, Rais wa Namibia Mh. Ifikepunye Pohamba na Mke wa Rais 
Mama Salma Kikwete wakiwa katika maadhimisho hayo
Vijana wa chipukizi wakionyesha michezo na ujumbe mbalimbali wakati wa maadhimisho hayo.
Hapa wakionyesha ukakamavu wao huku wakiwa wameshika silaha.
Kikosi
 cha wanaanga Jeshi la wananchi JWTZ kikitoa heshima kwa gwaride kali 
mbele ya Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jakmhuri ya Muungano ya Tanzania 
Dk. Jakaya Kikwete
Kikosi cha ardhini Jeshi la wananchi la Tanzania JWTZ kipita kwa gwaride la heshima mbele ya Rais Dk. Jakaya Kikwete.

















 
 
No comments:
Post a Comment