Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kulia)
akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe mara
baada ya kumtembelea ofisini kwake jana mjini Bukoba. Waziri Dk.
Mukangara yupo mkoani humo kwa ajili ya kuangalia jinsi fedha za mkopo
kutoka mfuko wa vijana zilivyoweza kuwasaidia vijana kujikwamua
kimaisha.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara
(kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian
Massawe alipomtembelea ofisini kwake jana mjini Bukoba. Waziri Dk.
Mukangara yupo mkoani humo kwa ajili ya kuangalia jinsi fedha za mkopo
kutoka mfuko wa vijana zilivyoweza kuwasaidia vijana kujikwamua
kimaisha.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kushoto
) akiongea na viongozi wa mkoa wa Kagera (hawapo pichani)jana mjini
Bukoba jinsi Serikali inavyoangalia uwezekano wa kuongea mkopo kwa
SACCOS zinazolenga shughuli za maendeleo ya vijana kutoka shilingi
milioni tano hadi kumi kutokana na mahitaji ya fedha hizo kuwa makubwa.
Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana James
Kajugusi.
Baadhi
ya viongozi wa mkoa wa Kagera wakimsikiliza Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (hayupo pichani) wakati
akiongea nao kuhusu umuhimu wa kuwafuatilia vijana kwa ukaribu katika
Kata na kuweza kuwafundisha na kuwashirikisha katika miradi ya
maendeleo,Picha na Anna Nkinda – Maelezo
Comments