Waziri
 Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa 
akipokelewa na viongozi wa Kanisa la Lutherani usharika wa 
Akyeri, Dayosisi ya Meru Mkoani Arusha kwa ajili ya kuongoza harambee ya 
kuchangia fedha kwa ajili ya ukarabati wa kanisa hilo, iliyofanyika leo 
Mkoani humo.
===========     =========   =========
Waziri
 Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa 
amesisitizia tena kuwa tatizo la ajira kwa vijana ni jambo la hatari kwa
 usalama wa nchi,wakati alipokuwa katika harambee ya kuchangia ukarabati
 wa kanisa la kilutheri usharika wa Akyeri Meru mkoani Arusha, Mh 
lowassa ameonya kuwa suala hilo lisiposhughulikiwa haraka litasababisha 
hali ya hatari.
”tunashuhudia
 maandamano katika mataifa ya ulaya vijana wakidai hali bora ya maisha 
pamoja na ajira.hali hiyo tusipoangalia inaweza kutokea hapa nchini 
kwetu.
huko
 nyuma niliwahi kusema kuwa makanisa, mashirika na watu binafsi wasaidie
 juhudi za serikali kutatua suala hilo”alisema Lowassa.
Lowassa
 ambaye katika harambee hiyo aliongozana na marafiki zake, ambapo yeye 
na familia yake pamoja na marafiki zake wamechangia kiasi cha shilingi 
millioni 33.2.
Zaidi ya shilingi millioni 160 zikiwa ni fedha tasilimu pamoja na ahadi zilipatikana katika harambee hiyo.
Kwa
 upande wake askofu Akyoo wa jimbo la Meru alimsifu Lowassa kwa 
uchapakazi wake popote alipokuwa.”Wakati ulipokuwa Waziri Mkuu 
ukimsaidia rais tulishuhudia uwezo wako mkubwa katika kufuatilia 
majukumu yako”alisema na kuongeza kuwa Lowassa ni mtu wa ibada
Waziri
 Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (wa tatu 
kushoto) akiongozana na Askofu wa Kanisha hilo la Lutherani usharika wa 
Akyeri, Dayosisi ya Meru Mkoani Arusha,Askofu Akyoo.
Waziri
 Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa 
akihutubia muda mfupi kabla ya kuanza kwa harambee ya kuchangia ujenzi 
wa Kanisa la Lutherani usharika wa Akyeri, Dayosisi ya Meru Mkoani 
Arusha.
Waziri
 Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipokea 
ahadi ya mchango kutoka kwa mmoja wa wamini wakati wa harambee ya 
kuchangia ujenzi wa Kanisa la Lutherani usharika wa Akyeri, Dayosisi ya 
Meru Mkoani Arusha.
Waziri
 Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiondoka
 kanisani hapo baada ya kumalizika kwa harambee ya kuchangia ujenzi wa 
Kanisa la Lutherani usharika wa Akyeri, Dayosisi ya Meru Mkoani Arusha.
 
 
No comments:
Post a Comment