Mambo makubwa yamefanyika katika uwanja wa CCM Kirumba usiku huu jijini Mwanza ambapo Kofii Olomide mwanamuziki
Gwiji Barani Afrika kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
amepagawisha mashabiki wa wake katika tamasha la Tusker Carnival na
kukonga nyoyo za mashabiki wa muziki jijini humo, Mwanamuziki Kofii
Olomide akiwa na kundi lake pamoja na mwimbaji wake Cindy amefanya
kilichokuwa kikitarajiwa pamoja na hamu ya mashabiki kupiga kelele kwa
madai ya kutaka kumuona mwanamuziki huyo mkali na anayekubalika barani
Afrika na Ulaya.
Mwanamuziki huyo amefanya mambo makubwa kama burudani aliyoshusha
jana kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam, Watu mbalimbali
wamejitokeza kwenye uwanja wa CCM Kirumba ili kumuona mwanamuziki huyo
pichani juu akiwa na mwimbaji wake Cindy akimtambulisha kwa mashabiki wa
jijini Mwanza .
Kamanda wa Fullshangblog
alikuwepo jijini Mwanza ili kukumuvuzishia moja kwa moja matukio hayo
usiku huu kutoka katika uwanja wa CCM Kirumba Kaa mkao wa kuperuzi mara
kwa mara katika ukurasa wa Fullshangwelog ili kujua kinachojiri uwanjani
hapo .
Kofii Olomide na Mwimbaji Cindy wakiimba huku wakiwa amezungukwa na wanenguaji wake
Mwanamuziki Kofii Olomide akipanda jukwaani huku akisinddikizwa na waimbaji wake.
Cindy
katikati Mwimbaji mahili wa kike wa mwanamuziki Kofii Olomide akiimba
jukwaani kalba ya Kofii Olomide mwenyewe kupanda jukwaani.
Kazi iko hapa kama wanavyoonekana wanenguaji hao wakicheza kwa sataili ya aina yake.
Hii ilichezwa kwa kwenda mbele na kurudi nyuma huku wakiwa wameshikana.
Palikuwa hapatoshi kwa shoo kabambe kabisa kutoka kwa wanenguaji wa Kofii Olomide.
Ili mradi burudani iliyopangika kutoka kwa wanenguaji hao
Staili hiyo ilichezwa kwa hisia pia
Kutoka
kulia ni Ephraim Mafuru Mkurugenzi wa Masoko wa (SBL), Anitha Msangi
Maurice Njowoka na Patrick Kisaka kutoka kampuni ya bia ya Serengeti
wakishoo love kwa picha.
Mkurugenzi
wa Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti Ephraim Mafuru kulia na
Mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga wakiwa katika picha ya
pamoja
Wadau kutoka Miss Tanzania wakiwa katika onesho hilo.
Rachel wa THT akicheza na mmoja wa wanenguaji wa mwanamuziki Kofii Olomide.
Kofii Olomide akimpongeza msanii Rachel wa THT baada ya kuonyesha uwezo wake katika kuimba kwenye onesho hilo.
Waimbaji wa mwanamuziki Kofii Olomide wakiimba kwa hisia katika enesho hilo.
Rapa wa mwanamuziki Kofii Olomide anayejulikana kwa jina la Computar akighani huku wanenguaji wa kiume wakiingia jukwaani.
Jukwaani ni Recho wa kundi la THT kutoka jijini Dar es salaam akinendelea kutoa burudani jukwaani
H.
Baba akifanya vitu vyake mbele ya mashabiki wa jijini Mwanza wakati
akitoa burudani ya utangulizi kabla ya mwanamuziki Kofii Olomide Kupanda
jukwaani.
Pepe Kale wa Mwanza naye akafanya mambo makubwa na kukubalika na umati wa mashabiki waliohudhuria katika onesho hilo. Kwa taarifa zaidi hebu cheki FULLSHANGWE.
Comments