Ze Comedy mambo bado


Pichani ni Kundi la Ze comedy wakishagilia kwa pamoja muda mfupi baada ya
Mahakama kuu kutupilia mbali ombi la EATV dhidi ya kikundi hicho..
--------
Na Emmanuel Mrema.
Mahakama Kuu,Kitengo cha Biashara imetupilia mbali pingamizi ya kituo cha televisheni cha EATV dhidi ya kikundi cha wachekeshaji cha Ze Comedy.Akisoma uamuzi huo,Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo Catherine Urio alisema pingamizi tatu zilizotolewa na EATV dhidi ya Ze Comedy hazina nguvu ya kuizuia mahakama isiendelee kuisikiliza kesi hiyo.Katika pingamizi hizo,EATV ilidai kuwa walalamikaji hawakuwa na sababu za msingi za kuwashitaki,hawakufuata taratibu za kisheria za kufungua kesi hiyo mahakamani na kwamba kiapo kilichotolewa na mshiriki mmoja kati ya wote hakijafuata taratibu za kisheria.
Jaji Urio alisema pingamizi la kwanza na la pili hajatolea uamuzi kwa kuwa unaingilia kesi ya msingi,lakini la tatu la kiapo kuna matatizo kidogo ambayo kisheria hayasumbui na kisheria inaruhusiwa waleta maombi kurekebisha kiapo hicho ili kesi iendelee kusikilizwa.
“Mahakama imeona ni vizuri warekebishe kiapo kingine ili haki itendeke kwa wote,”alisema Urio.Urio alisema mahakama itapokea maombi ya kiapo hicho kutoka kwa Ze Comedy Agosti mosi na Agosti 7 itapokea kutoka EATV ili iweze kukaa na kutolea uamuzi wake Agosti 15 mwaka huu.EATV inaongozwa na wakili wake Blandina Gogadi na Justin Kimaro wakati Ze Comedy inaongozwa na wakili Peter Swai.
Wasanii hao walikuwapo kusikiliza kesi yao ambao ni Emmanuel Mgaya‘Masanja’,Lucas Mhuvile‘Joti’Sekioni David‘Seki’,Mujuni Sylivery‘Mpoki’,Isaya Mwakilasa‘Wakuvanga’Alex Chalamila‘Mc Regan’na Joseph Shamba‘Vengu’.Kundi hilo lilikuwa likifanya maigizo katika Kituo cha EATV,lakini baada ya kumaliza mkataba wake na kuhamishia matangazo yake Televisheni ya Taifa,TBC1,limeingia katika matatizo baada ya kituo hicho kudai kuwa wao ndiyo wenye hakimiliki ya Ze Comedy.
Kundi hilo ambalo hivi karibuni lilitangaza kudhaminiwa na mfanyabiashara Yusuf Manji,lilifungua kesi katika Mahakama Kuu ya Kitengo cha Biashara, kuishitaki EATV na pia,likidai kulipwa Sh milioni 200 kutokana na kusababisha kutofanya kazi zake.

Comments

Anonymous said…
Some really superb information, Sword lily
I observed this. "Ideas control the world." by James Abram
Garfield.

Here is my page :: aimbot cod4
Anonymous said…
Very interesting information!Perfect just what I was looking for!

"Outside of a dog, a book is man's best friend. Inside of a dog it's too dark to read." by Groucho Marx.


My blog post: $20 PSN Card