Wednesday, July 16, 2008

Tume ya ghorofa yamkabidhi ripoti Kandoro


TUME iliyoundwa kuchunguza chanzo cha kuporomoka kwa jengo la ghorofa kumi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Abbas Kandoro jana imekabidhi rasmi taarifa kwa mkuu huyo wa mkoa baada ya kuomba kuongezewa wiki moja zaidi na kuwa na wiki tatu badala ya mbili awali.
Tume hiyo iliundwa ili kuchunguza chanzo cha kuporomoka kwa jengo la ghorofa kumi lililokuwa mtaa wa Mtendeni Manispaa ya Ilala katika Kata ya Kisutu imekabidhi kazi na kukiri kwamba ilikuwa ngumu sana.
Kandoro alisema anahitaji muda wa kutosha kuipitia kwa makini taarifa hiyo na atawasiliana na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu na ndipo serikali itakapotoa tamko.
"Taarifa hii itachanganywa na taarifa ya tume iliyoundwa na Waziri Mkuu kuchunguza jengo la hoteli ya Chang'ombe (Chang'ombe Village) lililobomoka mwaka juzi wilaya ya Temeke na kutolewa tamko kwa pamoja," alisema Kandoro
Alisema wananchi wawe na subira kwani katika taarifa ya tume hizo hakuna kitu kitakachofichwa badala yake zitafanyiwa kazi ili kuondoa tatizo hilo na taarifa zitatolewa kwa Umma. Habarri ya Ummy Muya.

No comments: