Taarifa zilizonifikia hivi punde ni kuwa gazeti la mwanahalisi limevamiwa
muda huu na polisi huku wanaendelea na upekuzi ila hatujui wanataka nini .
Waliwakuta ofisini ndugu Kubenea Said na Ndimara Tegambwagwe pamoja na mlizi
ndugu Mayunga.
Wanaendelea na upekuzi na itakumbuka kuwa hawa hawa ndio ambao walimwagiwa
tindikali na kesi bado inaendelea japo haijulikani nini hatima ya haya mambo
Wamechukua computer ambayo anaitumia pamoja na flash na wameondoka naye
kwenda kumsachi nyumbani kwake na hili lilitokana na kuwa polisi hawa
wanatafuta nyaraka fulani Kuna amri ya mahakama ya kufanya hivyo?
Taarifa tulizo nazo ni kwamba walikuwa wakitafuta nyaraka za benki zilizomuumbua mzee wa vijisenti na kumfanya ajiuzulu hali inayowafanya waingie kiwewe labda na wao siku moja haya mambo yatawakumba.
La maana ni kuwahi mahakamani (kama inawezekana) nadhani ndio sababu wamevamia late today... lakini kama wana search warrant na kama inawapa uwezo wa kwenda kusearch hadi nyumbani.
Upekuzi nyumbani kwake unaendelea na sasa haijulikani nini kinafanyika huko kwani simu yake haipokelewi tena .
Tutawapa yaliyojiri punde.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WIZARA YA AFYA YAOMBA SH. TRILIONI 1.8 BAJETI YA 2026/2027
Wizara ya Afya imeomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi trilioni 1.8 kwa mwaka wa fedha 2026/2027 kwa ajili ya kuendelea kuboresha huduma z...
-
Hapa mmoja wa watoto hao akiwa na kijana mwenzake mwenye miaka 18, wote wako sawa lakini yeye hawezi kuzungumza kama watu wa kawaida. Mama S...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
Pascal Mayalla akiwa katika chumba cha wagonjwa Daraja la kwanza katika hospitali ya mkoa wa Dodoma ambako amelazwa kwa matibabu baada ya ku...
No comments:
Post a Comment