Habari zingine bwana zinatisha sana kuna hizi habari kwamba huyu Rais wa Zambia Levy Mwanawasa amefariki dunia. Habari zilizotapakaa kila kona ya Dunia na wakati fulani kuthibitishwa na watu muhimu kama Thabo Mbeki na wengine kadhaa zinathibisha kifo cha huyu bwana ingawa kuna taarifa zinasema jamaa hajafa.
Rais Mwanawasa aliugua ghafla ugonjwa wa kiharusi wakati akihudhuria mkutano wa kilele wa wakuu wa Umoja wa Afrika huko Sharm el Sheikh Misri.
Makamu wa Rais wa Zambia Rupiah Banda amesema kuwa Rais Mwanawasa alipatwa na mshtuko kifuani muda mfupi kabla ya kuhudhuria kikao cha Baraza la usalama na amani la Umoja wa Afrika kabla ya kufunguliwa kwa mkutano huo.
Alisema kuwa kwa sasa amelazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi lakini hali yake inaendelea vizuri.
Hii ni mara ya pili kwa Rais huyo wa Zambia kupatwa na maradhi ya kiharusi, ambapo mara ya kwanza ilikuwa miaka miwili iliyopita.
Comments