MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini, (Sumatra), imepandisha nauli za mabasi nchini kote.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Sumatra jana jijini Dar es Salaam, nauli hizo ambazo zimepanda kwa zaidi ya asilimia 20 ya nauli za awali, zitaanza kutumika rasmi Agosti Mosi, mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Israel Sekirasa alisema uamuzi huo unatokana na kupanda kwa gharama za uendeshaji nchini.
"Kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta ya petroli na dizeli kufikia wastani wa Sh 1,700 kwa lita ya petroli na dizeli Sh2,000, ni lazima nauli ipande na hakuna jinsi ya kuepuka hali hiyo," alisema Sekirasa.
Comments