Ugeni wa WTO



MAKAMU wa Rais, Dk Ali Mohamed Shein, amesema misaada ya kifedha inayotolewa na wahisani kwa nchi zinazoendelea kwa ajili ya kuimarisha biashara isiwekewa masharti mazito ili kusaidia kukuza sekta hiyo katika nchi za kiafrika.

Dk Shein alisema hayo jana kwenye mkutano wa majadiliano ya jinsi ya kukusanya fedha kwa ajili ya misaada ya kimandeleo unaofanyika jijini Dar es Salaam, ambao umeandaliwa na Benki ya Maendeleo Afrika (ADB), Tume ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi kwa Afrika na Shirika la Biashara Duniani (WTO) kwa kushirikiana na Benki ya Dunia.

Alisema fedha hizo zinatakiwa pia kutolea kama msaada na siyo mikopo ili kuziwezesha nchi zinazopokea kufanikisha malengo yake katika kukuza biashara.

“Misaada ya kifedha kutoka kwa wahisani (AFT) inatakiwa kuwa ya uhakika na ipatikane kirahisi na kwa wakati badala ya kuwa na mlolongo mrefu unaombatana na mambo ya kisiasa, alisema Dk Shein.

Lengo la mjadala huo ni kuzihamasishga serikali, wafadhili na sekta binafsi kutoa changamoto sahihi kwa bara hili na kuweka bayana mahitaji na kushirikisha utatuzi wa matatizo na changamoto za kibiashara.

“Misaada yakifedha inayotolewa kwa ajili ya maendeleo lazima ilingane na mahitaji halisi ya walengwa,” alisitiza Dk Shein, kuongeza kuwa katika hilo kunahitajika kuwepo kwa mawasiliano sahihi na wapokeaji wa misaada hiyo iliiweze kuwa na manufaa wahusika.

Comments

Anonymous said…
aisee charahani ebu fanya advertisement ya nguvu kuhusu blog yako, aisee ni nzuri kweli! mimi ni mara yangu ya kwanza kuitembelea na nimeipenda sana.njia nzuri ni kuweka tangazo kwa bwana misupu ambaye amefanikiwa sana katika masuala haya ya blog kwa kuwa watu wengi wanatembelea blog yake. okay mr i wish you good luck.