Friday, October 19, 2007

Magari ya Zimamoto feki

Magari mawili ambayo yalinunuliwa na mwaka 2005 na Jiji la Dar es Salaam kwa zaidi ya Sh350 milioni yameshindwa kufanya kazi kutokana na kutopata usajili mpaka sasa.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam iliyosomwa kwa niaba yake na Afisa Muandamizi wa Zimamoto, Fikiri Salla kuwa kwa sasa kikosi hicho kina magari mawili tu yanayofanya kazi kati ya magari tisa yaliyopo.

"Hadi leo magari hayo hayajaanza kufanya kazi kutokana na malumbano yaliyopo kati ya Wizara ya Miundombinu na Manispaa ya Temeke, pamoja na ucheleweshwaji katika usajili wa gari la zimamoto la Manispaa ya Ilala.

Waandishi walishuhudia magari hayo yakiwa yameegeshwa katika makao Makuu ya kikosi hiho, huku moja likiwa halina namba na lingine likitumia namba injini (chasis nunmber)

Awali Mkuu wa Chuo hicho, Kamishina Msaidizi Omary Mrisi, alisema licha ya kupokea maombi kutoka nchi mbalimbali ya kujiunga na chuo hicho wameshindwa kuwapokea kutokana na uduni ya vitendea kazi.

Awali Kamati ya ya Ulinzi na Usalama ya Bunge iliyotembelea kikosi hicho imesema hali ya Kikosi cha Zimamoto nchini kimeshindwa kufanya kazi katika viwango vinavyostahili na kwamba hata chuo chake kikachotoa mafunzo ya zimamoto hakina hadhi.

Wabunge hao walisema hayo jana kamati hiyo ilipotembelea Makao Makuu ya kikosi hicho pamoja na Chuo cha Zimamoto ili kujionea shughuli zinazofanywa na kikosi hicho.

Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, na Mbunge wa Newala, Kapteni Goerge Mkuchika (CCM), alisema kuwa ni aibu kwa kikosi hicho kinachohudumia Jiji linalokadiriwa kuwa na watu milioni 3.5 kuwa na magari mabovu yasiyo na uwezo wa kutoa huduma hiyo.

Mkuchika alisema hayo kufuatia taarifa ya Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam iliyosomwa kwa niaba yake na Afisa Muandamizi wa Zimamoto, Fikiri Salla kuwa kwa sasa kikosi hicho kina magari mawili tu yanayofanya kazi kati ya magari tisa yaliyopo.

No comments: