Monday, October 29, 2007

Barrick Gold Tanania yatimua wafanyakazi 900

Kampuni ya Barrick Gold Tanzania leo imetangaza rasmi kuwa imewasimamisha kazi wafanyakazi takribani 900 katika mgodi wa wa Bulyanhulu uliopo Wilayani Kahama, Mkoani Shinyanga na siyo 700 kama ilivyokuwa .

Wafanyakaazi walioathirika na kusimamishwa kazi ni wale waliojisusisha na mgomo batili ulioitishwa na Chama cha Wafanyakazi wa Migodi na Ujenzi (TAMICO) jioni ya tarehe 24,October,2007.

Menejimenti ya mgodi wa Bulyanhulu imetoa taarifa kwa wafanyakazi wote ikiwaataarifu kuwa, wafanyakazi wote walioshindwa kurudi kazini kama walivyoagizwa wamesimamiswa kazi na nafasi zao zitatangazwa upya.

Menejimenti pia imefafanua kuwa waajiriwa wote wa hapo awali hawatabaguliwa kwa namna yeyote na kwamba kila mmoja anayo haki ya kuomba kazi kwa nafasi zitakazo tangazwa upya. habari zaidi soma hapa hebu mchekini Teweli Teweli anasemaje ili mpate taarifa zaidi.

No comments:

RAIS SAMIA ASHIRIKI NA KUTUNUKU TUZO ZA WASANII WA KOMEDI TANZANIA 2025

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameshiriki kama mgeni rasmi katika hafla ya utoaji wa Tuzo za Wasa...