Balozi wa Uholanzi anusurika ajalini



BALOZI wa Uholanzi nchini, Karel van Keresteren, amenusurika kwenye ajali ya gari iliyotokea mkoani Morogoro, Jumamosi wiki iliyopita baada ya gari yake kugongwa na lori la mizigo.

Balozi huyo pamoja na mkewe walikuwa njiani kuelekea mjini Morogoro ndipo walipopata ajali hiyo iliyotokea wakiwa karibu kufika mjini humo na kimsababishia Balozi Keresteren maumivu ya viungo.

Akizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Kitengo cha Uchumi na Biashara kwenye ubalozi wa nchi hiyo, Steef van den Berg, alisema balozi huyo alipata ajali hiyo Jumamosi majira ya saa saba mchana.

Alisema ajali hiyo ilitokea baada ya gari alilokuwa akisafiria balozi huyo kupita kwenye kizuizi cha Polisi wa Usalama Barabarani, ambapo lori hilo ambalo pia liliruhusiwa lililigonga kwa nyuma na kumsababishia mshituko katika baadhi ya maeneo ya mwili wake. Kwa taarifa zaidi soma Mwananchi

Comments