Tuesday, October 16, 2007

Aliyejenga hifadhi ya barabara kulipwa Sh15 bilioni

MAHAKAMA imeiamuru Serikali kuilipa kampuni ya Mansoor Oil Industries Ltd (MOIL) ya jijini Mwanza jumla ya Sh14.7bilioni
kutokana na uamuzi uliotolewa na Waziri wa Ujenzi wakati huo John Pombe Magufuli wa kuvunja kituo cha mafuta cha kampuni hiyo.

Uamuzi huo umetolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza katika kesi ya madai namba 2 ya mwaka 2002 ambapo
kampuni hiyo ilikuwa ikiwashitaki Waziri Magufuli, Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (wakati
huo) Brigedia Hassani Ngwilizi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Andrew Chenge pamoja na Halmashauri ya Jiji
la Mwanza.

Katika kesi hiyo madai ya kampuni hiyo ya MOIL kwa serikali yalikuwa jumla ya Sh.18bilioni kutokana na kuvunjiwa kituo hicho cha mafuta kilichokuwa kimejengwa katika kiwanja namba 178 Kitalu ‘A’ eneo la Kirumba kando ya barabara ya Makongoro.

Katika madai hayo, kampuni hiyo iliomba kulipwa kiasi cha Sh 593milioni kama thamani ya jengo ambalo lilibomolewa kwa amri ya Waziri Magufuli, Sh13.4 bilioni ikiwa ni kiasi cha faida ambacho ingekipata katika kipindi cha miaka 33 ambacho ilitarajiwa kufanya biashara na Sh 4 bilioni kama hasara ya jumla ya mradi huo. kwa taarifa zaidi soma Mwananchi

No comments: