Monday, October 22, 2007

Chissano anyakua tuzo ya Mo Ibrahim


RAIS mstaafu wa Msumbiji Joaqium Chissano, amewabwaga Marais wengine 12 akiwemo Benjamin Mkapa wa Tanzania, katika kinyang'anyiro cha Tuzo ya Rais bora wa Afrika.

Ushindi wa Chissano umetangazwa mjini London jana na Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa Mataifa (UN), Kofi Annan.

Tuzo hiyo ambayo imetolewa na Taasisi ya Mohamed Ibrahim, bilionea mzaliwa wa Sudan, msingi wake ni mambo matatu, Kukuza Demokrasi, Utawala Bora na Maendeleo katika nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Soma HAPA upate taarifa zaidi za kiongozi huyu wa Msumbiji.

No comments: