Monday, October 29, 2007

Jamani mama na watoto wazuri, baba hataki


Jamami hebu chekini binti mrembo watoto wazuri, lakini baba wa watoto hawataki, amewakimbia Binti huyu mkazi wa jijini Dar es Salaam, Tunu Mrisho (28), anaomba msaada wa matunzo ya watoto wake mapacha watatu baada ya mwanaume anayedai kuzaa naye kukataa kuhusika kumpa ujauzito wa watoto hao.

Tunu ambaye anaishi Kigogo First Inn kwa dada yake, Zubeda Hamisi, anadai kuwa mwanaume huyo (jina tunalo), mkazi wa kijiji cha Matombo, mkoani Morogoro, alikataa kuhusika kumpa ujauzito huo tangu ulipokuwa wa miezi mitano.

"Kabla ya hapo, (baba ya mapacha hao) alikuwa akifika nyumbani kama kawaida. Nilipobainika kuwa nina mimba ya miezi mitano, nilimweleza. Kufanya hivyo, akaacha kufika nyumbani na kuanzia siku hiyo sijamwona tena hadi sasa," alisema Tunu.

Akizungumza katika ofisi za Mwananchi Jumamosi wiki iliyopita, Tunu alisema mwanaume huyo alikataa kuhusika na suala hilo kwa maandishi mbele ya balozi wa nyumba kumi, kijijini hapo

No comments:

MAMA NEEMA MWIGULU AHIMIZA TAASISI KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI KUPITIA UWAJIBIKAJI KWA JAMII

Mwenza wa Waziri Mkuu, Mama Neema Mwigulu Nchemba, amehimiza taasisi za umma na binafsi kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kub...