Na Abdallah Nsabi wa Mwananchi
FURAHA ya ushindi wa Chama cha Mapinduzi CCM kupata ushindi wa Udiwani imemtokea puani mkazi wa kata ya Nguliguli Wilayani Maswa Lonjini Petro (54) baada ya kunywa lita tatu za pombe aina ya gongo na kufariki dunia.
   
Tukio hilo lilitokea juzi katika kata hiyo baada ya kutangazwa matokeo ya ushindi wa chama hicho ndipo Petro alipokwenda nyumbani kwa Gumba Mboje na kuangiza lita tatu za gongo ili anywe afurahie ushindi huo ambao alikuwa anausubiri kwa hamu na kukutwa na mauti.
   
Chanzo cha habari kutoka katika eneo hilo kilisema kuwa  Petro aliwekeana ahadi na mtu mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana kuwa iwapo chama cha CCM kingeshinda wangenunuliana pombe aina ya gongo na kunywa mpaka asubuhi.
   
Pia  ilieleza kuwa Mara baada ya ushindi wa chama cha Mapinduzi CCM, marehemu aliamua kujikita katika moja ya nyumba ambayo wanafanya biashara  hiyo na kisha kuanza kunywa pombe hiyo haramu hadi kukutwa na umauti papo papo.
   
Habari hizo zinaeleza kuwa  marehemu ambaye  enzi za uhai wake alikuwa kada wa chama hicho siku hiyo alionekana kuwa na furaha ya ushindi mara baada ya chama chake kutangazwa kushinda ndipo alipoamua kwenda kufakamia  kinywaji hicho kwa  majigambo kuwa  amefurahi kushinda kwa mgombea wao.
   
Wakazi wa kata hiyo mara baada ya  kumwona mwenzao amezidiwa kwa kinywaji hicho kutokana na kuanguka chini kwa kuzimia  walianza kumwagia maji ya baridi  huku wakimpepea  lakini  baada ya muda mfupi aliaga dunia.
   
Ilielezwa kuwa marehemu Petro alikuwa na kawaida ya kunywa pombe, lakini akuwahi kulewa sana kama ilivyotokea siku hiyo  ambayo alikuwa akisherehekea ushindi wa chama chake hicho alichokuwa  akikiunga mkono pamoja na kuwa na uanachama wa  muda mrefu.
   
Mbunge wa jimbo la Maswa John  Shibuda alithibitisha kutokea kwa kifo hicho cha mwanachama wa CCM na kuongeza kuwa hali hiyo ilimtokea wakati akishangilia ushindi  wa mgombea wa CCM.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
RAIS DKT. SAMIA AKUTANA NA UJUMBE WA JUKWAA LA MABUNGE LA NCHI ZA MAZIWA MAKUU (FP-ICGLR) IKULU NDOGO TUNGUU, ZANZIBAR
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Kiongozi wa Jukwaa la Mabunge la...
 
- 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
- 
Mwanamuziki toka Jamhuri ya KIdemokrasia ya Kongo, Mbilia Bel akitumbuiza katika viwanja vya bunge mjini Dodoma jana. Picha na Jube Tranquil...
- 
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
 
No comments:
Post a Comment