Wednesday, October 17, 2007

Mahakama yamwachia huru Lwakatare

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Kagera imemwachia huru Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Wilfred Lwakatale, katika shtaka lililokuwa likimkabili la kumshambulia na kumjeruhi Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Renatus Mutabuzi, kwa sharti la kutotenda kosa lolote la jinai ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu wa Mkazi wa mahakama hiyo, Cleophace Waane, baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashtaka na kwa kuzingatia maombi ya wakili wa mshtakiwa huyo, Twaha Tasilima, yaliyotolewa kabla ya hukumu hiyo kutolewa.

Akisoma hukumu hiyo, hakimu Waane alisema kuwa mahakama imeona baadhi ya maombi yaliyoombwa na wakili wa mshtakiwa ambayo aliomba yazingatiwe na mahakama wakati wa kutoa hukumu ni ya muhimu, hivyo kuamua kutoa adhabu ndogo kwa mshtakiwa huyo. Bonyeza GAZETI LA MWANANCHI upate taarifa zaidi.

No comments:

RAIS DKT. SAMIA AKUTANA NA UJUMBE WA JUKWAA LA MABUNGE LA NCHI ZA MAZIWA MAKUU (FP-ICGLR) IKULU NDOGO TUNGUU, ZANZIBAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Kiongozi wa Jukwaa la Mabunge la...