Gazeti jipya mtaani



Nimepata ujumbe ufuatao:-

Gazeti jipya kabisa la Kiswahili linatarajiwa kuingia katika vibanda, maofisi, na mitaa ya Tanzania kuanzia tarehe 31 Oktoba mwaka huu. Jarida hilo la "Raia Mwema" litakuwa na habari mbalimbali zikiwemo za uchunguzi, utafiti, siasa, biashara, maoni n.k Jarida hilo liitwalo "Raia Mwema" limeanzishwa kutokana michango ya hali, mali, na vipaji ambavyo vimekusanywa chini ya Mhariri wake Mtendaji John Bwire

Kuanzishwa kwa jarida hilo ni alama ya kuvunjika rasmi kwa ndoa ya gazeti lililosifika sana nchini miaka hiyo la "Rai".
Waandishi waanzilishi wa gazeti la Rai - ukiondoa Dr. Shoo na Salva - na waandishi wengine ndani na nje ya Tanzania wamefikia uamuzi wa kuanzisha gazeti hilo wakizingatia haja ya kupanua uhuru wa maoni, habari na mawazo na kuchangia kwa namna ya pekee kuhamasisha kizazi kipya cha "Raia Wema". Gazeti hilo litakuwa linatolewa kila wiki. Angalia mfano wake hapa: http://www.akili.biz/raiamwema/

Gazeti hilo litajumuisha waandishi mbalimbali wakiwemo:

Jenerali Ulimwengu
Issa Shivji
Padre Karugendo
Prof. Haroub Othman
Maggid Mjenga
Joseph Mihangwa

Na wenu mtiifu, na wengine wengi ambao mtapata bahati ya kusoma kazi zao kwenye gazeti hilo ambalo litapatikana pia kwenye mtandao wakati huo.

Napenda kutoa pongezi kwa ushirikiano wote wa wale ambao wamewezesha gazeti hili kupata mtaji, kibali, na nyenzo za kutendea kazi.. Natarajia kuwa toleo la kwanza litaiweka fani ya uandishi katika ngazi nyingine kabisa nchini.


Tafadhali copy na watumie wabongo walioko kwenye orodha yako ya anuani.

Ndugu yenu,

M. M.

Comments