Friday, January 08, 2016

MBWANA SAMATTA ATWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA AFRIKA
Mbwana Samatta ameitoa kimasomaso Tanzania kwa kutwaa tuzo ya Mchezaji bora wa mwaka anaechezea ligi za ndani itolewayo na CAF.
Mbwana Samatta usiku wa kuamkia ijumaa ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka Africa achezeaye ligi ya ndani itolewayo na CAF.

Samatta alikuwa akichuana na Baghdad Bounedjah wa Algeria na klabu ya Etoile du Sahel alietwaa nafasi nafasi ya tatu na Robert Kidiaba wa DR Congo na TP Mazembe alietwaa nafasi ya pili.

Samatta alikua na mwaka mzuri 2015 akiibuka kinara wa magoli katika ligi ya mabingwa Afrika sambamba na kutwaa Ubingwa huo na pia kushiriki katika klabu bingwa ya dunia.

Hongera Samatta, Hongera Tanzania.
Post a Comment