Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, leo tarehe 21 Mei 2026 amemtembelea na kumjulia hali Mwakilishi wa Viti Maalum kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Mhe. Farida Amour Moh’d, ambaye amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mjini Magharibi Lumumba kwa ajili ya matibabu.
Katika ziara hiyo, Mhe. Hemed alipata fursa ya kuzungumza na Mhe. Farida pamoja na madaktari wanaomuhudumia, ambapo alielezwa maendeleo ya afya yake na hatua zinazoendelea kuchukuliwa katika kumpatia huduma stahiki za matibabu.
Makamu wa Pili wa Rais alimtakia Mhe. Farida nafuu ya haraka na kurejea katika majukumu yake ya kuwahudumia wananchi, huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea kumpatia huduma bora za afya hadi atakapopona kikamilifu.
Ziara hiyo imeonesha mshikamano, upendo na utamaduni wa viongozi kujali ustawi wa wenzao wakati wa changamoto za kiafya.
Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)
Tarehe 21 Mei 2026.






No comments:
Post a Comment