Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimfariji Khadija Kianda mjane wa Marehemu Rajabu Kianda aliyekuwa mnikulu kufuatia kifo chake kilichotokea jumapili jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Khadija Kianda ambaye ni mjane wa Marehemu Rajabu Kianda aliyekuwa Mnikulu ambaye alifariki dunia Jumapili jijini Dar es Salaam.Rais Kikwete alikwenda nyumbani kwa marehemu eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam kuifariji familia ya marehemu ambaye anatarajia kuzikwa huko Kihurio Same,Mkoani Kilimanjaro.Pembeni ni Mama wa Marehemu ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza la aliyekuwa mnikulu Bwana Rajabu Kianda aliyefariki jana jijini Dar es Salaam.Marehemu Kianda anatarajiwa kuzikwa kesho nyumbani kwao Kihurio Same Mkoa wa Kilimanjaro.
(Picha na Freddy Maro)
**********************************************************************************************************
MNIKULU Rajabu Kianda, aliyefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu, atazikwa katika kijiji cha Kihurio wilayani Same, Kilimanjaro.
Kiyanda alifariki juzi mchana akiwa Hospital ya Taifa Muhimbili (MNH) alikopelekwa kwa matibabu.
Mwili wa Kianda uliagwa jana nyumbani kwake Mikocheni mara baada ya kumalizika kwa kisomo majira ya saa 8:00 mchana, kwa mujibu wa ndugu yake ambaye aliomba jina lake lisitajwe.
Kianda alianza kuugua tangu mwishoni mwa mwakaa jana nafasi yake inakaimiwa na Shabani Gurumo.
Kianda aliteuliwa kushika nafasi ya Mnikulu baada ya Anthony Itatiro kuhamishiwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Imeandikwa na Sadick Mtulya.
Comments